Ujumbe wa Faraja wa Ajibu kuelekea mechi dhidi ya Simba

Ujumbe wa Faraja wa Ajibu kuelekea mechi dhidi ya Simba

0

Ujumbe wa Faraja wa Ajibu kuelekea mechi dhidi ya Simba

SHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema mechi yao na Simba anaona ya kawaida huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho.

 

Kwa takriban siku nne ambazo Yanga imekuwa kambini mkoani Mo­rogoro, imekuwa ikifanya mazoezi ya nguvu na mbinu zaidi kuhakikisha Simba inakufa mapema hapo kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakao­chezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Ajibu ambaye amewahi kucheza Simba, ame­kuwa gumzo kutokana na kiwango chake kukua na mpaka sasa katika mechi nne alizocheza amefunga bao moja na kutoa pasi za mabao tano.

 

Mshambuliaji huyo, aliltuambia kuwa: “Mechi ni ya kawaida, kikubwa ni kujituma, kwa hiyo mashabiki wasiwe na hofu, dua zao zinahitajika zaidi ili tuweze kupata ush­indi kwenye mchezo huu.

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY