Ujumbe wa Mzee Akilimali kwenda kwa Haji Manara baada ya Kubanwa na...

Ujumbe wa Mzee Akilimali kwenda kwa Haji Manara baada ya Kubanwa na Ndanda

0

Ujumbe wa Mzee Akilimali kwenda kwa Haji Manara baada ya Kubanwa na Ndanda

Katibu wa baraza la wazee klabu ya Yanga mzee Ibrahim Akilimali ameibuka na Kumpa Ujumbe Afisa habari wa Simba Haji Manara baada ya Simba kubanwa na Ndanda Fc ya Mtwara katika mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu TPL.

Mzee Akilimali amemwambia Manara kupunguza Tambo na kuwa anawatania zaidi Yanga na kusahau kuwa Mpira huwa unamatokeo Matatu.

“Unajua huyu mdogo wangu nadhani bado hajaitambua ligi vizuri, namshauri tu vizuri kwa maana siwezi kumtania ni vema akaelewa kuwa mchezo una matokeo matatu. Namuomba apunguze zaidi tambo kwa timu yake na atambue kuwa si kila mechi unaweza kushinda”

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY