USAJILI : Anapoelekea Batambuze baada ya Kuondoka Singida United

USAJILI : Anapoelekea Batambuze baada ya Kuondoka Singida United

0

USAJILI : Anapoelekea Batambuze baada ya Kuondoka Singida United

Nairobi Kenya

Toka msimu mpya wa Ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL Msimu huu wa 2018/2019 uanze mchezaji Shafiq Batambuze wa Singida United hakurejea Tanzania na mpaka leo bado hajaungana na timu ya Singida United.

Sababu zinazotajwa ni kutokana na mchezaji huyo kutokamilishiwa stahiki zake na klabu ya Singida United kiasi cha kumfanya kuamua kuvunja mkataba na Singida United kwani alikuwa bado anamkataba wa mwaka mmoja.

Taarifa za Uhakika ambazo kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba mchezaji Shafiq Batambuze anayecheza kama beki wa Kushoto ameanza mazungumzo na Klabu ya Gor Mahia ya Kenya mazungumzo yanayotajwa yamefikia pazuri na muda wowote anaweza kutangazwa kama mrithi wa Mganda mwenzake Godfrey Walusimbi aliyetoka Gor Mahia na kujiunga Kazier Chief ya Afrika Kusini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY