Wachezaji wa Kuchungwa zaidi Uganda vs Tanzania/Taifa Stars leo

Wachezaji wa Kuchungwa zaidi Uganda vs Tanzania/Taifa Stars leo

0

Wachezaji wa Kuchungwa zaidi Uganda vs Tanzania/Taifa Stars leo

Ni wazi leo kutakuwa na moja ya mechi nzuri zaidi kuwahi kuzishuhudia kwa Taifa Stars kwani zinakutana timu majirani zenye baadhi ya wachezaji wanaofahamiana vyema.

Ongezeko la wachezaji wengi wanaocheza soka Nje ya nchi kunaweza kunogesha zaidi mchezo wa leo, Uganda wakiwaita Mapro wao zaidi ya 10 wakati Tanzania nao wakiwaita Mapro wao 9 kwenye timu ya Taifa.

Lakini je Umejiuliza ni wachezaji gani wanaoweza kuwa kivutio zaidi na bila shaka kuchungwa zaidi uwanjani?

Ebana asikuambie mtu kitu kuna maeneo kutakuwa kunamchuano mkali sana uwanjani.

Upande wa Uganda kuna wachezaji ambao ni hatari kwa safu ya Ulinzi ya Taifa Stars kutokana na Ubora walionao wachezaji hao wachezaji kama Emmanuel Okwi ambaye anacheza Tanzania katika klabu ya SImba na Farouk Miya anayecheza HNK Gorica ya Croatia.Image result for farouk miya

Ukiachana na wachezaji hao Ubora wa Winga wa Kushoto wa Uganda KIZITO ambaye anasifika kwa kasi yake na krosi anazopiga kila anapopanda kushambulia.

Lakini upande wa Tanzania wachezaji hatari wa Kuchungwa ni Mbwana Samatta ambaye amekuwa na kiwango bora siku za Karibuni akiichezea klabu yake ya Genk ya Nchini Ubelgiji.

Lakini pia uwepo wa mchezaji kama Thomas Ulimwengu unaweza ukawa hatari kwa mabeki wa Uganda kwani Ulimwengu na Samatta wamekuwa na Combination nzuri wanapocheza pamoja toka wakiwa TP Mazembe.

Lakini uwepo pia wa mchezaji kama Shaban Chilunda ambaye Waganda wengi wanaweza wasimtilie maanani sana inaweza ikawa hatari kwa waganda bila kujua.

Battle kubwa ambazo zinaweza kutokea uwanjani leo.

Juuko v Samatta

Okwi v Aggrey Morris

Kizito v Kessy

Aucho v Himid (Eneo la katikati ya uwanja)

Miya v Banda

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY