Watakaotemwa Yanga dirisha dogo hawa hapa

Watakaotemwa Yanga dirisha dogo hawa hapa

0

Watakaotemwa Yanga dirisha dogo hawa hapa

Kocha Mwinyi Zahera unaambiwa anataka kuisuka Yanga ambayo itakuwa tishio Tanzania msimu huu na baadaye kuwa Tishio barani Afrika kutokana na makali itakayokuwa nayo.

Kutokana na hilo habari za ndani kutoka Yanga msomaji wa kwataunit.co.ke inaelezwa kuwa kocha huyo ameshapeleka mamombi ya kuwataka nyota kadhaa watakaoisaidia Yanga kipindi ambacho dirisha dogo litafunguliwa.

Huku baadhi ya nyota wa Yanga wakitajwa kuwa wapo kwenye hatari ya kuachwa kwenye kikosi cha Yanga kutokana na majeruhi ya mara kwa mara lakini pia uwezo wao kuonekana kushuka ndani ya Kikosi cha Yanga.

Kwa mujibu wa chanzo chetu wachezaji Thaban Kamusoko na Amis Tamwe wapo kwenye hatari zaidi ya Kuachwa kwenye dirisha Dogo huku mambo yakikaa sawa nyota kutoka TP Mazembe Ben Malongo anayecheza kama mshambuliaji anaweza kumrithi Tambwe

Wakati Fabrice Ngoma AS Vita anayecheza kama kiungo akitajwa huenda akamrithi Kamusoko wachezaji hao wote wapo kwenye timu ya taifa ya Congo ambayo Mwinyi Zahera ni kocha msaidizi wa timu hiyo. Kuzipata habari kwa wakati like Ukurasa wetu wa Facebook HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY