Wawili Rayon watajwa Simba akiwemo mbaya wa Yanga

Wawili Rayon watajwa Simba akiwemo mbaya wa Yanga

0

Wawili Rayon watajwa Simba akiwemo mbaya wa Yanga

UNAMKUMBUKA yule Mnyarwanda anayekipiga katika klabu ya Ryon Sports, aliyeimaliza Yanga kwa kuifunga bao la kiufundi katika dakika ya 18 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hivi karibuni?

Basi jina lake anaitwa Caleb Bimenyimana, ambaye duru za kimichezo zinasema kwamba huenda straika huyo akakipiga katika klabu ya Simba hapo baadaye endapo mipango ya kusaini kuichezea klabu hiyo itafanikiwa.

Habari hizo zinasema Bimenyimana anatarajia kusajili katika klabu hiyo bingwa ya Tanzania katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo, ambapo mipango yote inasukwa na straika wa timu hiyo, Meddy Kagere, ambaye kwa sasa yupo Rwanda akiitumikia timu ya Taifa ya nchi hiyo, Amavubi.

Kocha msaidizi wa Simba ambaye aliwahi kuifundisha klabu anayochezea Bimenyimana, alikataa kuzungumzia lolote kuhusu straika huyo, akidai kwamba taratibu za kazi hazimruhusu kuzungumzia hilo, lakini taarifa ambazo tunazo ni kwamba, kocha anamkubali sana straika huyo anayefanya vizuri hivi sasa katika klabu yake.

Licha ya straika huyo anayetajwa kuwaniwa na Simba, vilevile nyota mwingine katika kikosi hicho, Ismaila Diarra, naye anatajwa kuwamo katika mawindo ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Source : Dimba

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY