Yanga ilimsajili mchezaji aliyefungiwa na CAF ndo maana hachezi

Yanga ilimsajili mchezaji aliyefungiwa na CAF ndo maana hachezi

0

Yanga ilisajili mchezaji aliyefungiwa na CAF ndo maana hachezi

Wakati taarifa zikisema kuwa sababu za Mohammed Issa Banka kutokucheza ni kutokana na kuuguza Magoti yake huko kwa Zanzibar taarifa mpya zimeibuka kuhusu ni nini hasa kinachofanya mchezaji huyo kutocheza mpaka leo.

Taarifa za kuaminika ambazo kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba Mohammed Issa Banka alifungukiwa na CAF kutokana na vipimo vyake kukutwa anatumia madawa yaliyokatazwa michezoni.

Vipimo hivyo vilichukuliwa wakati timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ilikuwa inashiriki michuano ya CECAFA mwaka jana huko nchini Kenya na Baada ya vipimo akagundulika kuwa anatumia dawa hizo na CAF wakawa wamemfungia mwaka mmoja.

Taarifa zaidi zinasema kuwa TFF waliambiwa na CAF na TFF wakawaambia Mtibwa Sugar ambao waliacha kumtumia mchezaji huyo Toka February 2018 lakini Yanga kwakutokujijua Hili walimsajili Mohammed Issa Banka bila kujua haya.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY