Yanga ingekutana na wabaya wa Simba kama wangefuzu makundi CAF

Yanga ingekutana na wabaya wa Simba kama wangefuzu makundi CAF

0

Yanga ingekutana na wabaya wa Simba kama wangefuzu makundi CAF

Kama Yanga ingefanikiwa kufuzu hatua ya Makundi Kombe la shirikisho barani Afrika CAF basi ingekutana na timu ambazo zimewahi kuitoa Simba katika michuano ya Afrika ngazi ya Vilabu.

Ikumbukwe Yanga ilikuwa Kundi D na timu nyingine za USM Alger, Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya ambapo timu za USM Alger ya ALgeria ilifanikiwa kuongoza kundi na Kufuatiwa na Rayon Sports.

Katika Droo ya robo fainali USM Alger wamejikuta wakidondoka mikononi mwa El Masry ya Misri nao Rayon Sports imedondoka kwa Enyimba ya Nigeria.

Kwahiyo kama Yanga ingefuzu hatua Hiyo basi ingekutana na moja ya timu hizo ambazo zimewahi kuitoa Simba Enyimba ya Nigeria au El Masry ya Misri.

ROBO FAINALI ITAKUWA HIVI.

Rayon Sports (Rwanda ) vs Enyimba (Nigeria)
CARA (Congo) vs Raja Club Athletic (Morocco)
El Masry (Egypt) vs USM Alger (Algeria)
AS Vita (DR Congo) vs RS Berkane (Morocco)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY