Yanga kuwakosa nyota wake wanne mchezo na Coastal Union

Yanga kuwakosa nyota wake wanne mchezo na Coastal Union

0

Yanga kuwakosa nyota wake wanne mchezo na Coastal Union

Jumatano ya 19.9.2018 Kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kucheza na Coastal Union katika uwanja wa Taifa ikiwa ni mechi ya Tatu kwa Yanga ya Kwanza ikishinda mbele ya Mtibwa 2 kwa 1, Ya Pili ikishinda bao 4 kwa 3 dhidi ya Stand United.

Kuelekea mechi hiyo ya Kesho Jumatano  Yanga itawakosa wachezaji wake wanne kutokana na Sababu mbalimbali.

Wachezaji hao ni Juma MAHADHI ambaye bado hajawa fiti asilimia mia moja licha ya kuanza mazoezi mepesi ambayo amekuwa akisimamiwa na Daktari.

Wengine ni wachezaji watatu ambao walitimuliwa na Kocha Mwinyi Zahera baada ya Kutotii maagizo ya Kuwepo uwanjani kwenye mchezo kati ya Yanga na Stand United.

Wachezaji hao ambao walitakiwa kukaa jukwaani kuwaangalia wenzao ni Haji Mwinyi, Said Makapu na Pius Buswita ambao walikacha na Kutotokea uwanjani siku ya Mchezo huo, Zahera aliwatimua na kuwaambia watarejea kambini baada ya mechi ya Jumatano.Kwa habari za Kila wakati kwa haraka Like Ukurasa wetu wa Facebook HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY