Yanga yatajwa chanzo cha Masoud Juma Kubaki Dar, ishu iko Hivi

Yanga yatajwa chanzo cha Masoud Juma Kubaki Dar, ishu iko Hivi

0

Yanga yatajwa chanzo cha Masoud Juma Kubaki Dar, ishu iko Hivi

Wakati wadau wengi wa soka wakiwa bado haiwaingii akilini sababu hasa iliyotolewa ya kocha Masoud Djuma kusalia jijini Dar Es Salaam ikielezwa ni kwaajili ya kubaki na wachezaji walioachwa safari ya Mtwara kuna jipya limeibuka juu ya kwanini hasa Masoud Amesalia Dar.

Kwa Mujibu wa taarifa za Uhakika ambazo kwataunit.co.ke imezipata kutoka kwa watu wa karibu kabisa wa Simba inaelezwa kuwa Kocha Masoud Djuma kubakia Dar ni kwasababu ya Yanga.

ISHU IKO HIVI.

Kila mtu anatambua kuwa September 30 2018 kutakuwa na mchezo kati ya Simba na Yanga sasa kocha Aussems alifanya maamuzi ya Kumuacha Masoud Djuma ili afatilie mchezo wa Yanga na Stand United ili kuwasoma zaidi Yanga kabla ya kukutana nao. Kuzipata habari za Michezo kila wakati Like Ukurasa wetu wa Facebook HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY