Abdi Banda amshangaa Ibrahim Ajibu

Abdi Banda amshangaa Ibrahim Ajibu

0

Abdi Banda amshangaa Ibrahim Ajibu

Wakati goli la Ibrahim Ajibu likiendelea kuwa gumzo maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Mipaka ya Tanzania, Beki wa Kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la Kulipwa nchini Afrika Kusini Abdi Banda amemshangaa Ibrahim Ajibu.

Abdi Banda amemshangaa Ibrahim Ajibu kuendelea kucheza soka lake nchini Tanzania kwani anaamini uwezo wa Ibrahim Ajibu ni mkubwa kiasi cha kucheza soka nchi yoyote ile kama atakuwa tayari.

Abdi Banda alifunguka kuwa anaamini sana kwenye uwezo wa Ajibu na anaona ameshafanya kila kitu kwenye soka la Tanzania kwahiyo kwasasa ni bora akaanza kufikiria kutoka nje ya Nchi ili kutafuta changamoto mpya za Kisoka.

Abdi Banda kwasasa amekuwa moja ya wachezaji wanaoaminiwa kwenye kikosi cha Baroka Fc inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY