Adhabu walizopewa Kotei na Andrew Vincent hizi hapa

Adhabu walizopewa Kotei na Andrew Vincent hizi hapa

0

Adhabu walizopewa Kotei na Andrew Vincent hizi hapa

Hatimaye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka nchini Tanzani TFF limetoa maamuzi juu ya wachezaji James Kotei wa Simba na Andrew Vincent wa Yanga.

Wachezaji hao wamejikuta wakiangukiwa na Nyundo ya Kamati ya Nidhamu kwa kufungiwa mechi 3 za Ligi kuu na faini ya Laki tano

Kotei anafungiwa kutokana na Kumpiga ngumi Gadiel Michael wa Yanga huku Andrew Vincent akikumbana na adhabu hiyo kutokana na Kumpiga kichwa Zimbwe Jr, maarufu kama Tshabalala katika mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga

Kanuni namba 38 kifungu cha tatu ya udhibiti wa wachezaji inasema “Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga/kupigana atasimama kushiriki michezo mitatu (3) ya klabu yake na atalipa faini ya Sh 500,000,”

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY