Aussems ataja kocha msaidizi anayemtaka Simba

Aussems ataja kocha msaidizi anayemtaka Simba

0

Aussems ataja kocha msaidizi anayemtaka Simba

Siku kadhaa toka klabu ya Simba kupitia kwa kaimu rais wa Klabu hiyo Salim Abdallah Try Again kutangaza rasmi kuachana na kocha wake msaidizi Mburundi Masoud Djuma mapya yameibuka juu ya Kocha ambaye atakuja kurithi mikoba ya Masoud Djuma.

Kocha mkuu Patrick Aussems ameeleza sifa za kocha msaidizi anayemtaka kuwa ni lazima awe mzawa yani Mtanzania kwakuwa imekuwa utaratibu wake popote anapofanya kazi

Lakini pia ni lazima awe ni kocha atakayekuwa akimsikiliza, kocha anayejua majukumu yake lakini pia ni lazima awe kocha mwenye hamu ya mafanikio.

HAWA WANATAJWA ZAIDI.

Licha ya kuwa yeye hatamchagua lakini inaelezwa kuna majina ya makocha watatu wazawa inaelezwa kuwa kocha Amri Said wa Mbao Fc au Suleiman Matola wa Lipuli Fc mmoja wapo huenda akachua nafasi kama kocha msaidizi wa Simba

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY