Habari njema kwa wanaSimba leo 10.10.2018

Habari njema kwa wanaSimba leo 10.10.2018

0

Habari njema kwa wanaSimba leo 10.10.2018

Baada ya Kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu hatimaye kiungo mchezeshaji wa Simba Hassan Dilunga HD jana ameanza mazoezi rasmi na wachezaji wenzake wa Simba.

Habari hii ni njema kwa washabiki, wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba kwani Dilunga ni moja ya viungo ambao katika michezo waliyoitumikia Simba walionyesha viwango vya Juu sana kwa kutoa pasi za Usaidizi na Kufunga pia.

Hassan Dilunga aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kati ya Simba na AFC Leopards mechi iliyochezwa September 8 uwanja wa Taifa Simba Ikishinda Bao 4 kwa 2 na nafasi ya Dilunga ikichukuliwa na Said Ndemla dakika ya 56.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY