Hii hapa Ishu ya Yusuph Manji kurejea Yanga Rasmi

Hii hapa Ishu ya Yusuph Manji kurejea Yanga Rasmi

0

Hii hapa Ishu ya Yusuph Manji kurejea Yanga Rasmi

Wakati watu wakiwa bado wako katika Sintofahamu juu ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kama amerejea kweli au bado ni Story tu.

Manji kwa mara ya Kwanza alionekana kurejea Yanga alipoibuka uwanja wa Taifa Yanga ikiwalaza waarabu kombe la Shirikisho barani Afrika kwa bao 2 kwa 1 LAKINI baada ya hapo ukimya ukatanda.

Mechi 3 za Leo Ligi Kuu TPL

Taarifa za ndani ambazo kwataunit.co.ke imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa klabu ya Yanga zinasema kuwa kamati ya Uchaguzi klabu ya Yanga ni kama wameshatoa majibu juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa Yusuph Manji ndani ya yanga.

Ishu iko Hivi 

Kamati hiyo ya Uchaguzi inaelezwa kuwa imepanga kufanya uchaguzi wa Yanga November 24 lakini katika nafasi zinazotakiwa kugombewa nafasi ya Mwenyekiti haipo, na zilizopo ni nafasi ya Kaimu mwenyekiti, na wajumbe waliojiuzulu.

Baada ya kutokuwepo kwa nafasi ya Kugombea kwa mwenyekiti inaashiria kuwa Yusuph Manji bado nafasi yake ipo na Inatambulika na inawezekana kamati ya Uchaguzi imeshakaa naye na Kukubaliana naye ndiyo maana wameonelea wasiweke nafasi hiyo katika uchaguzi huo kwakuwa inamtu ambaye ni Yusuph Manji. Kuendelea kuzipata habari za Yanga kiurahisi Install Application yetu ya kwataunit HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY