Kitenge aliyewaua Yanga aandaliwa kuia Simba kocha afunguka

Kitenge aliyewaua Yanga aandaliwa kuia Simba kocha afunguka

0

Kitenge aliyewaua Yanga aandaliwa kuia Simba kocha afunguka

KOCHA msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal ‘Bilo’, amesema wanaendelea kumwandaa mshambuliaji wake, Ale Kitenge, ili aweze kufunga mabao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaochezwa Oktoba 21, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza nasi jana kwa simu kutoka Shinyanga, Bilo alisema kikosi chake kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo, lakini akitumia muda mwingi kutengeneza makali ya mshambuliaji huyo.

Bilo alisema wanaendelea kumpa mbinu mpya kwani mabeki wamekuwa wakimkaba mno na kushindwa kufunga hasa baada ya kufunga dhidi ya Yanga.

Alisema kutokana na mshambuliaji huyo kukamiwa na mabeki wengi, wameamua kumpa mbinu mpya ili kukabiliana na changamoto hiyo.

“Kitenge hajashuka, makali yake ni yale yale, kilichomrudisha nyuma ni mabeki wengi kumkamia, umeona kila mechi tunayocheza anawekewa ulinzi mkali ila tumepata dawa na mechi ya Simba atafunga,” alisema Bilo.

Bilo alisema timu ilikuwa Kahama ambako waliweka kambi na kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Bulyankuru inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

credit : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY