Kocha anayetajwa kumrithi Masoud Djuma huyu hapa mwenyewe afunguka haya

Kocha anayetajwa kumrithi Masoud Djuma huyu hapa mwenyewe afunguka haya

0

Kocha anayetajwa kumrithi Masoud Djuma huyu hapa mwenyewe afunguka haya

Siku moja baada ya Klabu ya Simba kumtimua kocha wake msaidizi Masoud Djuma raia wa Burundi kutokana na kutoelewana na kocha Mkuu.

Taarifa za chini kwa chini ambazo kwataunit.co.ke imezinasa ni kwamba Simba inatajwa kuwa katika mipango ya kuinasa saini ya kocha wa sasa wa Mbao Fc Amri Said ili kuirithi mikoba ya Masoud Djuma.

Amri Said amewahi kuwa mchezaji wa Simba, Meneja lakini pia kocha msaidizi ambapo kwasasa ni kocha anayeiongoza Mbao Fc akiibuka pia kuwa kocha Bora wa mwezi TPL.

MWENYEWE AFUNGUKA.

Baada ya Tetesi hizo Amri Said Mwenyewe amefunguka kuwa mpaka sasa hajafanya mazungumzo na klabu ya Simba kwani alikuwa busy na Mchezo dhidi ya Yanga lakini yeye kama mwajiriwa wa Mbao Fc kwasasa kama kutakuwa na Taarifa anaamini atapokea kutoka kwa Viongozi wake.

Lakini yuko tayari kujiunga na Simba kama watahitaji huduma yake,

“Nipo na Uongozi wangu kama kuna Taarifa yoyote wataniambia ila kwasasa sina Taarifa yoyote, Mimi kama Mwalimu siwezi kusema sitaki mimi nipo kwaajili ya kufanya kazi na Simba ni Taasisi kubwa nimefanya kazi hapo nimekaa kwa muda mrefu”

Ikumbukwe pia msomaji wa Kwataunit.co.ke  Amri Said ndiye kocha Pekee aliyefanikiwa Kuifunga Simba msimu huu ambapo alikiongoza kikosi cha Mbao Fc kupata Ushindi wa bao 1 kwa 0 CCM Kirumba.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY