Maneno ya Okwi kuhusu Kipa Beno Kakolanya

Maneno ya Okwi kuhusu Kipa Beno Kakolanya

0

Maneno ya Okwi kuhusu Kipa Beno Kakolanya

Mara baada ya Mchezo kati ya Simba na Yanga kumalizika kwa Sare ya bila kufungana ni mengi sana yameandikwa na kuongelea kuhusu uwezo wa kipa wa Yanga Beno Kakolanya.

Lakini unajua wachezaji wa Simba wamemwongeleaje mchezaji huyo aliyeonekana kuwa kikwazo kwa Simba?

Emmanuel Okwi ambaye ni moja kati ya Washambuliaji hatari nchini Tanzania kwenye ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPL amemwangia sifa kipa huyo kwa Kusema kuwa alikuwa katika kiwango bora na aliweza kuwasoma washambuliaji wa Simba kabla na wakati wa Kushambulia.

Okwi pia alifunguka kuwa walicheza vizuri lakini walikosa bahati ya Ushindi.

“ tumecheza vizuri lakini hatukuwa na bahati ya ushindi. Naweza sema kipa wao alitusoma vyema kabla na wakati wa kushambulia “

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY