Mashindano ya Basketball NBL kanda ya Nyanda za Juu Fainali kuchezwa leo

Mashindano ya Basketball NBL kanda ya Nyanda za Juu Fainali kuchezwa leo

0

Mashindano ya Basketball NBL kanda ya Nyanda za Juu Fainali kuchezwa leo

Mashindano ya siku mbili ya Mchezo wa Kikapu kwa nyanda za juu Kusini kwa mabingwa wa mikoa ya nyanda za Juu kusini inayohusisha mikoa ya Mbeya , Iringa , Njombe na Rukwa ilianza jana na leo itafikia tamati.

Mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa Basket wa Roman Catholic Youthe Centre lengo lake ni kutafuta timu mbili ambazo zitawakilisha kanda katika michuano ya klabu bingwa Taifa ilianza jana ambapo Timu zinazoshiriki ni tano

Timu hizo ambazo ni Young Warriors na Buffalo kutoka Mkoa wa Iringa, Home Boys kutoka Mkoani Rukwa na wawakilishi wa mkoa wa Mbeya Mbeya Super Team wakiwa ndiyo mabingwa wa mkoa wa Mbeya na Makamu bingwa Mbeya Flames kwa wanaume na wanawake zinashiriki timu mbili pekee ambazo ni Mbeya na Iringa.

Baada ya mechi za jana ambapo leo zitachezwa mechi za kumalizia hatua ya Kwanza na Kisha zitafuata mechi za nusu Fainali na Fainali yenyewe.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY