Mgawanyo wa mapato na kiasi walichopata Simba

Mgawanyo wa mapato na kiasi walichopata Simba

0

Mgawanyo wa mapato na kiasi walichopata Simba

Dar es Salaam. Klabu ya Simba imepata kiasi cha shilingi 194,962,105.41 za mchezo wao na Yanga wa jana Jumapili ya Septemba 30, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kama wenyeji.

Simba imepata kiasi hicho kati ya shilingi  404,549,000 zilizopatikana katika mchezo huo namba 72, wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL)  baada ya kuingiza jumla ya watazamaji 50,168 kwa sababu ni wenyeji na

Yanga haijaambulia kitu.

Mgawanyo wa mapato hayo umefanyika kwa upande wa VAT, Selcom, TFF, Uwanja, Simba, TPLB, gharama za mchezo, BMT na DRFA.

Kati ya fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi milioni 61,710,864.41, Selcom milioni 17,901,293.25.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) milioni 16,246,842.12,Uwanja milioni 48,740,526.35.

Wenyeji wa mchezo Simba milioni 194,962,105.41, TPLB milioni 29,244,315.81,gharama ya mchezo 22,745,578.96, BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27.

Source : Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY