Simba wataja wachezaji wawili watakaokosekana dhidi ya African Lyon Leo

Simba wataja wachezaji wawili watakaokosekana dhidi ya African Lyon Leo

0

Simba wataja wachezaji wawili watakaokosekana dhidi ya African Lyon Leo

Klabu ya Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Sunday Manara imetaja wazi wachezaji ambao watakosekana kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya African Lyon utakaochezwa leo uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.

Haji Manara amewataja wachezaji hao kuwa ni John Bocco ambaye anatumikia kadi nyekundu na Hassan Dilunga ambaye majeruhi yake bado hayajatengemaa kisawasawa.

Manara amefunguka pia kuwa wachezaji waliokuwa timu ya taifa wamerejeshwa kikosini kwahiyo itakuwa ni maamuzi ya kocha kuwatumia au kutowatumia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY