Tetesi za usajili barani Ulaya leo 16.10.2018

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 16.10.2018

0

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 16.10.2018

Mshindi wa Olimpiki mara nane katika mbio za mita 100 Usain Bolt, 32, amepewa kandarasi ya miaka miwili kuchezea klabu ya Valletta FC ya Malta. (ESPN)

Manchester United imepuuzilia mbali madai kwamba klabu hiyo huenda ikauzwa hivi karibuni. (Mirror)

Barcelona imeungana na United katika kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Tottenham na timu ya taifa ya Ubelgiji oby Alderweireld, 29. (Mirror)

 

United na Spurs watasubiri kuona ikiwa Chelsea itajaribu kumsajili tena kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Nathan Ake, 23, na iwapo itaendelea na azma yake ya kumsajili mlinzi huyo wa Bournemouth. (Telegraph)

Manchester city ina haki ya kumliki tena winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho , baada ya kunyimwa kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza kwa mara ya kwanza. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27, yuko wa huru kujiunga na mahasimu sita wakuu wa Arsenal akiamua kuondoka Emirates bila malipo katika msimu wa joto. (ESPN)

 

Chelsea iko tayari kutumia Euro milioni 20 (£17.6m) kumpata kiungo wa kati wa Brescia mataliano Sandro Tonali, 28, katika dirisha la uhamisho. (Calciomercato)

Liverpool wanammezea mate mshambuliaji wa Napoli na Italia Lorenzo Insigne, 27. (Rai Sport – via Sun)

Southampton, Crystal Palace na Cardiff wanamfuatilia mshambuliaji wa Roma mzaliwa wa Bosnia Edin Dzeko, 32, ambaye anataka kurudi katika ligi kuu ya England. (Mirror)

Beki wa Uhispania Alberto Moreno, 26, anajiandaa kuondoka Liverpool kwa uhamisho bila malipo mwisho wa msimu huu. (Goal)

 

Newcastle inapania kumsajili winga wa Verde Garry Rodrigues, 27, kutoka Galatasaray. (Hurriyet – in Turkish)

Mlinzi wa Everton Phil Jagielka, 36, huenda akaondoka klabu hiyo kadarasi yake ikimalizika mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo)

Winga wa Ubelgiji Kevin Mirallas, 31, hana mpango wa kurejea Everton kibarua chake cha kuchezea Fiorentina kwa mkopo kitakapo malizika. (La Nazione – in Italian)

Mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny, 33, amesema alikuwa anashabikia Croatia kisiri dhidi ya taifa lake Ufaransa katika fainali ya kombe la Dunia baada ya kuachwa nje ya kikosi hicho kutokana na jeraha. (Canal Plus, via Goal.com)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY