Tetesi za usajili barani Ulaya leo 18 October 2018

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 18 October 2018

0

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 18 October 2018

West Ham inatafakari uhamisho wa mwezi Januari wa mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 32. (Mirror)

Nyota wa Brazil Neymar, 26, anajutia uamuzi wake wa kuondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain na kwamba yuka radhi kurejea Nou Camp mwisho wa msimu huu. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)

Wachezaji mahiri wa Ufaransa katika klabu ya Barcelona wanamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kujiunga na klabu hiyo. (Mail)

Andreas Pereira, 22, wa Manchester United amethibitisha majibizano makali kati ya Pogba na meneja wake Jose Mourinho yalitokana na tofauti kuhusiana na video katika mtando wa kijamii wa Instagram. (Manchester Evening News)

 

Mfaransa mwenzake katika klabu hiyo, Hugo Lloris anasema kuwa Pogba anahukumiwa kimakosa kwa sababu ya thamani yake ya euro milioni 89m. (Mirror)

Manchester United na Liverpool wanamfuatilia winga wa PSV Steven Bergwijn wa miaka 21. (De Telegraaf, via Sun)

Arsenal ni klabu ya hivi punde kuhusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Italia na Cagliari, Nicolo Barella, 21. (Gazetta dello Sport, via Football London)

Vilabu vya Juventus, Barcelona na Manchester City vinapania kumnunua mlinzi wa Ajax Matthijs De Ligt,19, ambaye huenda akagharimu karibu euro milioni 50. (Goal.com)

Agenti wa mlinzi wa Juventu, Daniele Rugani, anadai kuwa mchezaji huyo wa kimatafa wa Italia mwenye umri wa miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea msimu uliopita wa joto. (Calciomercato)

 

Tetesi za kuhusishwa kwa mlinzi wa kimataifa wa Slovakia na Inter Milan, Milan Skriniar, 23, na vilabu vya Manchester United na Manchester City, zinaashiria kiungo huyo huenda akajiunga na ligi ya Primia. (La Gazetta, via Calciomercato)

Tottenham inatarajia kufungua sehemu ya kwanza ya uwanja wao kwa umma jumamosi hii. (London Evening Standard)

Manchester City huenda ikasalia bila kiungo wa Brazil Danilo kwa angalau mwezi mmoja baada ya beki huyo wa miaka 27 kuumia alipokua akiichezea timu yake ya taifa wiki hii. (Globo Esporte, via Manchester Evening News)

Meneja wa Everton Marco Silva amesema “Manahodha wangu wawili” Phil Jagielka, 36, na Leighton Baines, 33, bado wana majukumu muhimu ya kufanya katika klabu hiyo- na kusisitiza kuwa mashauriano kuhusu kandarasi mpya ziwekwe kando kwa ajili ya siku zijazo. (Liverpool Echo)

 

Kiungo wa zamani wa Arsenal Paul Merson anasema endapo mchezaji wa miaka 27 wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey ataruhusiwa kuondoka Gunners bila malip itakuwa “kawaida Arsenal”. (Talksport)

Mlinzi wa zamani wa Manchester United Patrice Evra, anadai kuwa hata meneja wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson, alikua akijumuika nae kucheza densi katika chumba cha kubadilisha nguo. (Mail)

Mipango inafanywa kumkumbuka mwanzilishi wa Arsenal David Danskin. Alizikwa katika kaburi lisilojulikana katika Coventry lakini klabu ya Arsenal inatarajia kuandaa ibada ya wafu mwaka ujao. (Coventry Telegraph)

credit : bbc

Waliodownload App yetu kaa chonjo muda wowote Tutakuwa Tukitoa zawadi za Vocha, Kama bado haujadownload BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY