TFF yashangaa malalamiko haya ya Kocha wa Simba

TFF yashangaa malalamiko haya ya Kocha wa Simba

0

TFF yashangaa malalamiko haya ya Kocha wa Simba

SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemshangaa kocha wa Simba, raia wa Ubelgji Patrick Aussems aliyedai kwamba wachezaji wake wanapewa mazoezi makali ndani ya Taifa Stars ndio maana wanapata majeraha.

Aussems aliwashushia lawama hizo TFF baada ya mchezo wa Simba na Africa Lyon kwa akiwataja zaidi Shomari Kapombe na Jonas Mkude.

Lakini Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa ni jambo la ajabu hasa kwa mwalimu kusema kuwa mazoezi yanawaumiza wachezaji kwani wanajengwa kwa mazoezi.

 

“Uwezo wa mchezaji unaongezeka kutokana na mazoezi na kama wao wanalalamika suala hilo basi kuna tatizo hasa kwa wachezaji wenyewe kuwa wavivu kufanya mazoezi ama mazoezi wanayopewa ni rahisi hivyo wamekutana na ugumu ambao umewashtua.

 

“Timu ipo kwenye maandalizi ya kucheza na Cape Verde hivyo uimara unahitajika ili wachezaji waweze kupambana kiasi kikubwa na kama watafanya mazoezi kidogo jambo hilo halileti afya kwenye soka la ushindani,” alisema Ndimbo.

source : GPL

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY