Tundaman : Asema yeye Simba ila bao la Ajibu ……

Tundaman : Asema yeye Simba ila bao la Ajibu ……

0

Tundaman : Asema yeye Simba ila bao la Ajibu ……

Msanii wa Bongofleva na shabiki mkubwa wa klabu ya Simba, Tundaman, ameweka pembeni ushabiki wake na kuungana na nyota wa Yanga Ibrahim Ajibu , akimpongeza kwa bao lake la jana dhidi ya Mbao FC.

Tundaman ambaye ni mkali wa ‘hit’ nyingi ukiwemo wimbo wa Simba, amesema bao la Ajibu jana usiku ndio bao bora la msimu huu na shughuli ya kutafuta bao bora imefungwa fundi huyo wa soka.

”Mimi simba damu ila goli la msimu huu limeshafungwa jana na mwanangu fundi Ibrahim Ajibu, cha msingi wachezaji wafanye vitu vingine”, amesema.

Ajibu jana aliifungia Yanga bao la pili kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa mtindo wa ‘Bicycle Kick/Acrobatic’ na bao hilo limekuwa gumzo mtandaoni.

Ibrahim Ajibu alihamia Yanga msimu wa 2017/18 akitokea Simba  ambayo aliichezea kuanzia timu za vijana ngazi mbalimbali mpaka timu ya wakubwa.

source :EATV

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY