USAJILI : Chirwa azidi kuwachanganya Yanga

USAJILI : Chirwa azidi kuwachanganya Yanga

0

USAJILI : Chirwa azidi kuwachanganya Yanga

Wakati wapo wanaoamini kuwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa atarejea Yanga na kuungana na safu ya Ushambuliaji wa Yanga inayoongozwa na Heritier Makambo straika huyo amezidi kuwavuruga wanaYanga.

Kuwavuruga huko wanaYanga kunatokana na Post ambazo amekuwa akizipost Straika huyo bila kuwa na maelezo ya Kutosha alianza kwa kumpost Kocha wa sasa wa Azam Fc Hans Van Pluijm

Kisha baadae akaja kumpost straika mwenzake kipindi wapo Yanga Donald Ngoma ambaye naye yupo Azam Fc mara baada ya mchezaji huyo kupona na kurejea katika mechi kati ya Azam na Lipuli

Lakini kama haitoshi Chirwa  msomaji wa Kwataunit.co.ke siku moja baada ya mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga alipost picha akiwa amevaa uzi wa Azam Fc matukio haya yamezidi kuwavuruga wanaYanga kwenye mitandao ya Kijamii huku zikiwemo tetesi za mchezaji huyo huenda akatua Azam Fc kuungana na kocha wake wa zamani Pluijm wakati wa dirisha dogo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY