USAJILI: Mpishi wa Magoli ya Kagere aziita Simba na Yanga

USAJILI: Mpishi wa Magoli ya Kagere aziita Simba na Yanga

0

USAJILI: Mpishi wa Magoli ya Kagere aziita Simba na Yanga

Wakati timu mbalimbali zikiwa tayari zimeshaanza kuwa na mipango mbalimbali ya kuimaridha vikosi vyao wakati wa dirisha dogo huenda battle ya usajili Simba na Yanga ikarejea tena.

Hii inatokana na wakati wa dirisha kubwa hali hiyo kuonekana licha ya Simba kufanikiwa zaidi kuwin Battle hiyo ya Usajili kwa kuwasajili wengi ambao Yanga pia iliwahitaji.

Unamkumbuka Francis Kahata ? Yes huyu ni kiungo mchezeshaji wa Gor Mahia ya kenya ambaye mara nyingi alikuwa akimfanya Meddie Kagere kuwika kutokana na pasi zake murua alizokuwa mara nyingi akimpigia wakicheza K’Ogalo Gor Mahia.

Sasa habari za uhakika ambazo kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba kiungo huyo amemaliza mkataba na Gor Mahia na sasa anatamani kucheza soka Tanzania katika vilabu viwili vikubwa nchini Simba au Yanga.

Simba na Yanga zote ziliwahi kumwitaji kiungo huyo ambaye anauwezo mkubwa wa kucheza vizuri eneo la kati ya uwanja huku akisifika kwa pasi za mwisho lakini pia hata Kufunga kwahiyo kumalizika kwa mkataba na Gor Mahia na kutamani kwake kucheza Tanzania ni nafasi kwa Simba na Yanga kuweza kufanya naye mazungumzo.Kuzipata habari punde tu zinapotoka kwenye simu yako kama Inavyoingia Meseji Download Application yetu HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY