USAJILI: Simba yaingilia dili la Yanga kumsajili nyota huyu

USAJILI: Simba yaingilia dili la Yanga kumsajili nyota huyu

0

USAJILI: Simba yaingilia dili la Yanga kumsajili nyota huyu

Wakati dirisha dogo likiwa liko mbioni kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Maarufu kama TPL tayari timu mbalimbali zimeanza kutoa macho kuangalia nyota wa kuwaongeza na kuwapunguza kwenye vikosi vyao kulingana na mahitaji ya waalimu.

Moja ya vilabu ambavyo tayari vimeshaanza juhudi za kuhakikisha vinaongeza na kupunguza wachezaji ni Simba Na Yanga.

Yanga siku kadhaa zilizopita walitajwa kuwa katika mipango ya Kuinasa saini ya Straika wa Mbeya City Eliud AMBOKILE ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao kwasasa Ligi Kuu TPL akiwa na magoli 7 mpaka sasa.

Lakini dili hilo kwa taarifa za uhakika ambazo kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba Simba nao wameingia kwenye rada kama za Yanga za kuitaka saini ya Eliud Ambokile.

Lakini Simba wao wakiwa wanamuhitaji kama kiungo wa pembeni namba 7 au 11 tofauti na Yanga ambao wanamtaka kama mshambuliaji wa Kati kusaidiana na Heritier Makambo.

Simba inaelezwa wanamhitaji mchezaji mwenye kasi anayeweza kutokea pembeni kitu ambacho Eliud Ambokile anacho na tayari yupo katika majina yaliyopendekezwa ili aweze kusajiliwa.

naye Ambokile mwenyewe amefunguka kuwa yeye kwasasa bado anamkataba na Mbeya City mkataba wa miezi 6 umebaki hivyo kama kunatimu inamhitaji basi wafanye kuwasiliana na uongozi ambao ndiyo wamiliki wa mchezaji huyo.Kuzipata habari punde tu zinapotoka kwenye simu yako kama Inavyoingia Meseji Download Application yetu HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY