Yanga wafunguka hali ya Beno Kakolanya baada ya kuumia jana

Yanga wafunguka hali ya Beno Kakolanya baada ya kuumia jana

0

Yanga wafunguka hali ya Beno Kakolanya baada ya kuumia jana

Jana kulikuwa na pamban kati ya Yanga na Mbao fc katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2 kwa 0.

Katika mchezo huo kipa namba moja wa Yanga Beno Kakolanya alishindwa kumaliza pambano hilo mara baada ya dakika ya 55 kutoka baada ya Kuumia na nafasi yake kuchukiwa na Mkongo Klaus Kindoki.

Baada ya hali hiyo Msomaji wa kwataunit.co.ke  washabiki na wapenzi wengi wa Yanga waliingiwa hofu kutokana na Kakolanya kutolewa nje kwaajili ya matibabu zaidi kabla ya baadaye kurudi uwanjani na kukaa benchi.

Afisa habarI msaidizi wa Timu ya Yanga Godlisten Chicharito baada ya mechi hiyo aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Kipa Beno kakolanya yupo sawa na amerejea timu ya Taifa

Golikipa @official_beno_kakolanya18 yupo sawa na tayari amerejea kambi ya timu ya taifa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY