Alichokisema Thomas Ulimwengu baada ya kutajwa kutua Simba

Alichokisema Thomas Ulimwengu baada ya kutajwa kutua Simba

0

Alichokisema Thomas Ulimwengu baada ya kutajwa kutua Simba

Siku kadhaa baada ya Thomas Ulimwengu kutajwa kuwa huenda akatua katika klabu ya Simba wakati wa Dirisha dogo mwenyewe amefunguka kitu kuhusiana na tetesi hizo.

Thomas Ulimwengu ambaye kwasasa yupo kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars AFRIKA KUSINI inayojiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho amefunguka kuwa kwasasa hawezi kuongea chochote kuhusu usajili wake kwani akili ipo kwenye timu ya Taifa.

Ulimwengu amefunguka zaidi kuwa watu wasubirie ataongelea kila kitu kuhusu usajili wake na timu atakayokwenda wakati utakapofika.

“Hakuna ninachoweza kusema kuhusu usajili wangu, akili yangu ipo timu ya taifa tu wakati huo hayo mengine yakiendelea huko. Kama kutakuwa na lolote nitaliweka wazi  ila kwasasa naomba mniache kwanza,’ alisema Ulimwengu.

Siku kadhaa zilizopita Thomas Ulimwengu alivunja mkataba wake na klabu aliyokuwa akiichezea ya Al Hilal ya Sudan na kwasasa ni mchezaji huru.Punguza Matumizi ya MB Download App Bora Ya Michezo na Utumie MB chache tu tofauti na Kawaida BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY