Asante Kwasi aamua kuchukua maamuzi magumu Simba

Asante Kwasi aamua kuchukua maamuzi magumu Simba

0

BEKI wa kushoto wa Simba, Asante Kwasi, raia wa Ghana, amefanya maamuzi magumu baada ya kuondoka nchini kwenda kwao Ghana kujitibu majera aliyonayo.

Beki huyo amejikuta akipata majeraha mara mbili mfululizo, hali inayomfanya kuweka rehani namba yake kwa mwenzake, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye amekuja na moto mkali.

Akizungumza nasi hivi karibuni, Kwasi alisema anakwenda nyumbani kwa ajili ya kusalimia familia, lakini pia kuangalia afya ambayo imekuwa ikimsumbua kwa muda sasa.

Kwasi hakuweka wazi atarudi kikosini baada ya muda gani, hususan kwenye kipindi hiki ambacho ligi inatarajia kusimama, ila alisisitiza kwamba anakwenda kuangalia afya yake.

ìNinakwenda nyumbani, sijajua ni lini nitarudi, ninaangalia afya yangu kwanza nikiwa pamoja na familia yangu,  alisema.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussem, alithibisha kuondoka kwa mchezaji huyo, akidai amempa ruhusa kwenda kujiuguza nyumbani.

ìKwasi anaumwa na ameomba ruhusa aende nyumbani kuangalia familia na afya yake, nadhani hilo halina tatizo, kwani ameomba ruhusa, alisema

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY