Tetesi za usajili ulaya leo Jumanne 13.11.2018

Tetesi za usajili ulaya leo Jumanne 13.11.2018

0

Tetesi za usajili ulaya leo Jumanne 13.11.2018

Hatua ya meneja wa Manchester United Jose Mourinho kumchagua kiungo wa kati Nemanja Matic,30, imeendelea kuzua maswali miongoni mwa baadhi ya wachezaji wenzake wa kimataifa kutoka Serbia. (Times – subscription required)

Mpango wa aliyekuwa kiungo wa kati wa Ufaransa Samir Nasri kuhamia West Ham uko mashakani kufuatia hali ya kiafya ya kiungo huyu wa miaka 31. (Daily Mirror)

Santiago Solari anatarajiwa kuteuliwa meneja wa Real Madrid kwa mkataba utakaoendelea hadi mwisho wa msimu ujao. (Marca – in Spanish)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Ubelgiji Mousa Dembele amesafiri nchini Qatar kwa matibabu maalum ya kifundo cha mguu . (Evening Standard)

 

Aliyekuwa meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema atasubiri hadi msimu wa joto kuanza kazi yake mpya . (Rai Sport, via Goal)

Uamuzi wa Conte kusubiri inamaanisha Chelsea huenda ikamlipa euro milioni 11 kama fidia – hii ikiwa inajumuisha pesa zote alizokuwa alipwe meneja huyo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake. (Daily Mirror)

Vilabu vinavyoshiriki ligi ya primia vitaruhusiwa kuwasajili wachezaji 12 wa ulaya katika vikosi vyaovya wachezaji 25 chini ya kanuni mpya ya shirikisho la soka linapojiandaa katika mpango wa Uingereza kujiondoa kutoka Muungano wa Ulayo mchakato naofahamika kama Brexit. (Times)

 

Vilabu vya Borussia Dortmund na Marseille vinapania kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Ben Cottrell, alaiye na umri wa miaka 17.(Sun)

Beki wa Paris St-Germain Dani Alves,35, amesema amedokeza azma yake ya kucheza ligi ya primia kabla astaafu. (Daily Telegraph)

Meneja wa Arsenal Unai Emery na wachezaji wake walizungumza na mshambuliaji wa Gunners na England aliyeumia Danny Welbeck katika ujumbe wa video kabla ya mechi yao ya Jumapili dhidi ya Wolves ambapo walitoka sare ya bao 1-1. (Guardian)

Kungo wa kati na mshambuliaji hodari wa Manchester City Kevin de Bruyne anatazamiwa kurejea uwanjani mapema kuliko ilivyotarajiwa baada ya kupona goti lake. (Guardian)

Tetesi za Usajili Yanga 13.11.2018

Brighton inatarajiwa kukata rufaa ya kupinga kadi nyekundi iliyopewa kiungo wake wa kati Dale Stephen katika mechi ya siku ya siku ya Jumamosi ambapo waliinyuka Cardiff mabao 2-1. (Argus)

Klabu ya Al-Jazira kutoka Milki ya Kiarabu UAE inapania kumteua Michael Reiziger kama meneja kocha wake.

Reiziger amabaye alikuwa mlinzi wa zamani wa Ajax, Barcelona na Middlesbrough kwa sasa anasimamimia wachezaji wa ziada wa Ajax. (De Telegraaf – in Dutch)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY