Walichokisema Ndanda kuhusu Vitalis Mayanga kutua Yanga

Walichokisema Ndanda kuhusu Vitalis Mayanga kutua Yanga

0

Walichokisema Ndanda kuhusu Vitalis Mayanga kutua Yanga

Kocha wa timu ya Ndanda FC, Malale Hamsini amesema kama Yanga wanamhitaji mshambuliaji Vitalis Mayanga wafuate utaratibu ili wapewe mshambuliaji huyo kwenye usajili wa dirisha dogo utakaofunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15.

Mayanga ana mabao 5 mpaka sasa kwenye ligi, hivi karibuni alimpiga chenga kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kabla ya kutoa pasi ya bao kwa Nassor Saleh, amejizolea umaarufu kutokana na kazi kubwa aliyoifanya.

Alichokisema Thomas Ulimwengu baada ya tetesi za Kutua Simba

“Kama Yanga wanamhitaji Mayanga, wafuate tu utaratibu, sisi hatuwezi kumzuia mchezaji yeyote kwani soka ndiyo ajira yao, sasa timu kubwa kama Yanga inamhitaji hatuna kinyongo ila inabidi wajue bado ana mkataba,” alisema.

Mwinyi Zahera ambaye ni kocha mkuu wa Yanga aliwahi kukiri kuwa anahitaji saini ya nyota huyo ili aweze kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji kwa kusaidiana na Heritier Makambo na Amiss Tambwe.Punguza Matumizi ya MB Download App Bora Ya Michezo na Utumie MB chache tu tofauti na Kawaida BONYEZA HAPA

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY