Zahera afunguka usajili wa Beki Rayon kumbe ishu iko Hivi

Zahera afunguka usajili wa Beki Rayon kumbe ishu iko Hivi

0

Zahera afunguka usajili wa Beki Rayon kumbe ishu iko Hivi

Mwezi Agosti mwaka huu Yanga ilicheza mechi ya kukamilisha ratiba michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika 29 Agosti 2018 ikicheza dhidi ya Rayon Sports.

Katika mchezo huo Yanga ilipoteza kwa bao moja kwa sifuri bao la Rayon Sports likifungwa na Bimenyimana katika dakika ya 19 huku kikwazo kikubwa kwa Yanga kutopata bao katika mchezo huo ikiwa ni safu ya Ulinzi ya Rayon iliyoongozwa na beki Abdul Rwatubyaye.

Alichokisema Thomas Ulimwengu baada ya tetesi za Kutua Simba

Baada ya mchezo huo beki huyo alionekana katika picha akiwa na kamati ya usajili klabu ya Yanga ikiongozwa na Hussein Nyika na kuzua taarifa nyingi za Yanga kuwa katika mchakato wa kumsajili.

Lakini kocha wa Yanga Zahera mwinyi amekanusha taarifa za Yanga kuwa katika mipango ya kumsajili nyota huyo wa Rayon Sports.

Zahera alisema hata yeye amekuwa akiona tu habari kwenye magazeti na vyombo vya habari ilhali yeye hana taarifa hizo na hata viongozi wa Yanga hawajawahi kuongea naye juu ya suala la usajili wa beki huyo raia wa Rwanda..Punguza Matumizi ya MB Download App Bora Ya Michezo na Utumie MB chache tu tofauti na Kawaida BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY