Habari mpya waliyoitoa Yanga kuelekea mchezo na Biashara

Habari mpya waliyoitoa Yanga kuelekea mchezo na Biashara

0

Habari mpya waliyoitoa Yanga kuelekea mchezo na Biashara

Yanga kupitia KURASA zake za Mitandao ya Kijamii wameandika Ujumbe wa Mambo machache aliyozungumza Kocha Mwinyi Zahera kuelekea mchezo dhidi ya Biashara United Kesho 9.12.2018 ikiwemo hali ya wachezaji na wachezaji watakaokosekana.

MACHACHE YA KOCHA MKUU KUELEKEA MCHEZO WA KESHO “Wachezaji watatu wamerejea kwenye kikosi na watakuwa sehemu ya mchezo wa kesho,Papy Tshishimbi,Gadiel Michael na Kelvin Yondani.” “Wachezaji Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngasa wao moja kwa moja hawatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho ila Heritier Makambo ana asilimia 50 kwenye kushiriki mchezo wa kesho baada ya kupata maumivu kwenye mazoezi ya leo” “Tumejiandaa vyema kuwakabili Biashara maana mara zote unapocheza na hizi timu ndogo amabazo zipo chini kwenye msimamo zinakamia sana ivyo tumejiandaa vyema kuwakabili” Mwinyi Zahera – Kocha Mkuu #mabingwawakihistoria🇹🇿

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY