Huyu ndiye Ibrahim Hamid usajili mpya Yanga na nafasi anayocheza

Huyu ndiye Ibrahim Hamid usajili mpya Yanga na nafasi anayocheza

0

Huyu ndiye Ibrahim Hamid usajili mpya Yanga na nafasi anayocheza

Kama utani vile ila unaweza usiamini ila Beno Kakolanya ndiyo hivyo anaondoka Yanga kwani wapo waliojiuliza sana kuhusu kama kaachwa mbona hajaandikwa kwenye list ya walioachwa?

Lakini Yanga katika wachezaji wawili iliyowaongeza mmoja ni nafasi ya Golikipa ambayo alikuwa akicheza Beno kabla ya Kocha Zahera Mwinyi kumwambia atafute timu.

Habari mpya kutoka Simba leo 16 December 2018

Katika majina mawili yaliyoongezwa na Yanga yupo Haruna Moshi Boban ambaye anajulikana lakini kuna jina ambalo watu wengi hawalijui ambalo ni Ibrahim Hamid.

Ibrahim Hamid msomaji wa Kwataunit.co.ke ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Beach Soccer akitoka kuwakilisha nchi kwenye AFCON ya Beach Soccer huko nchini Misri.

Walioachwa na kusajiliwa Yanga dirisha Dogo

Ni kijana aliyezaliwa 10 April 1994 akiwa ni raia wa Tanzania na anacheza nafasi ya Kipa. Licha ya kuwepo Juma Kaseja katika timu ya Beach Soccer lakini huyu mara nyingi ndiye amekuwa chaguo la Kwanza la Kocha Boniface Pawasa.

Kipa huyo hajawahi kucheza timu kubwa za madaraja ya juu na badala yake amewahi kuwa kipa wa Manzese United ya Jijini Dar Es Salaam

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY