Kaheza ataka jezi ya Wanga

Kaheza ataka jezi ya Wanga

0

Kaheza ataka jezi ya Wanga

STRAIKA wa Simba, Marcel Kaheza aliyejiunga na AFC Leopards ya Kenya kwa mkopo, amesema anapenda kuvaa jezi namba 11 au 10 katika kikosi hicho.

Akiwa Simba, Kaheza alikuwa anatumia jezi namba 11 ambayo katika timu ya AFC Leopads ilikuwa ikivaliwa na Allan Wanga aliyewahi kukipiga Azam FC kwa sasa  amejiunga na Kakamega.

Mabingwa Klabu Bingwa Afrika toka 2003 mpaka 2018

Akizungumza nasi juzi kwa simu kutoka Kenya, Kaheza alisema katika timu hiyo mpya angependa kuendelea kutumia jezi namba 11 aliyokuwa anatumia Simba.

“Hadi Jumatatu (leo) nitajua navaa jezi namba ngapi, lakini nimependekeza 11 au 10, ndiyo ninazozipenda kwa sababu nimezitumia huko nyuma,” alisema Kaheza.

Alisema kama hiyo itakuwa na mtu anaomba namba 10 aliyoitumia kwa muda mrefu wakati akiwa Majimaji kwa sababu ni namba zinazomvutia.

 Kaheza alisema amejiandaa kwa ushindani wa Ligi Kuu Kenya na kuhakikisha anapata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY