Kaizer Chief Yamtangaza Ernst Middendorp kuwa Kocha Mpya
Moja kati ya Vilabu vikubwa nchini Afrika Kusini Klabu ya Kaizer Chief maarufu pia kama Amakhosi wamemtangaza kocha wao mpya.
Kaizer Chief wamemtangaza Ernst Middendorp KUWA kocha mpya wa Klabu hiyo kwa mkataba wa Miaka miwili na nusu kuitumikia Kaizer Chief.
Kaizer Chief wametangaza pia kuwa kocha msaidizi atatangazwa baadae .
Kaizer Chief walitangaza kuvunja mkataba na Makocha waliokuwepo ambao ni Giovanni Solinas ambaye alikuwa kocha Mkuu na Kisha baadae kutangaza kuvunja mkataba na Kocha msaidizi Patrick Mabedi
Kupitia Ukurasa wao wa Twitter Kaizer Chief waliandika.
Middendorp appointed as new coach
Kaizer Chiefs can confirm the appointment of Ernst Middendorp as the new head coach on a deal for two and a half years.
Welcome back to the Amakhosi Family#HailTheChief #Amakhosi4Life pic.twitter.com/3ZHuXTSDaO
— Kaizer Chiefs (@KaizerChiefs) December 7, 2018