Matokeo Tanzania Prisons vs Yanga leo 3 December 2018
Matokeo ya Mechi kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga leo 3 December 2018 moja kwa moja kutoka uwanja wa Sokoine Mbeya.
Mechi inaenda kuanza saa kumi kamili alasiri
Mechi Imeanza
Tanzania Prisons 0 – 0 Yanga
Dakika ya 4 Ibrahim Ajibu anajaribu shuti linaenda nje ya lango
Dakika 8 za Awali Yanga wameshacheza madhambi mara tatu
Tanzania Prisons 0 – 0 Yanga
Dakika ya 10 Krosi ya Mrisho Ngassa inashindwa kutumiwa vyema na Heritier Makambo.
Dakika ya 13 Tanzania Prisons wanatengeneza shambulizi zuri Ramadhan Kabwili anaokoa shambulizi.
Dakika ya 14 Yanga wanapata Kona
Dakika 15
Tanzania Prisons 0 – 0 Yanga
Dakika ya 17 Yanga wanapata mpira wa adhabu nje kidogo ya 18
Dakika ya ya 19 Makambo anaanguka baada ya kuguswa kidogo ndani ya 18 refa anapeta.
Dakika ya 20 Prisons wanapata Kona
Dakika ya 23 Prisons wanapata tena Kona baada ya kutengeneza Shambulizi
Kikosi cha Prisons dhi ya Yanga
Dakika 25
Tanzania Prisons 0 – 0 Yanga
Timu zote zinashindwa kutua nafasi inazotengeneza, Matokeo yakiwa bado 0 kwa 0
Dakika ya 33 Yanga wanafanya shambulizi jingine shuti la Ibrahim Ajibu linakosa madhara kwa Prisons.
Dakika ya 35 Maka Edward anapewa kadi baada ya kumchezea rafu Kelvin Friday, Mpira wa adhabu kuelekea Yanga
Dakika 40
Tanzania Prisons 0 – 0 Yanga
Dakika ya 41 Ibrahim Ajibu anaangushwa kwenye 18 Refa Meshack Suda anapeta
Dakika ya 43 Refa anawapa Tuta Tanzania Prisons
Wachezaji wa Yanga wanaonekana kumzonga mwamuzi Meshack Suda anawapa wachezaji watatu wa Yanga kadi za Njano, Juma Abdul na Ibrahim Ajib
Goaaaaaal Dakika ya 45 Jumanne Elifadhil anaipatia Prisons goli kwa njia ya penati
Tanzania Prisons 1 – 0 Yanga
Mrisho Ngassa na Laurian Mpalile wanapewa kadi nyekundu
Zimetokea Vurugu nyingi sana kabla ya kipindi cha Kwanza kumalizika hasa baada ya penati kutolewa
HALF TIME
Tanzania Prisons 1 – 0 Yanga
KIPINDI CHA PILI
Matheo Anthony anaingia kuchukua nafasi ya Maka Edward
Dakika ya 47 Yanga wanapata free kick inapigwa na Ajibu kipa anatoa na Kuwa Kona
Dakika ya 52 Jumanne Elifadhili anapewa kadi ya njano
Dakika ya 64 Yanga wanacheza Free kick lakini mpira Unatoka nje na Kuwa Goal Kick
Dakika ya 68 Feisal Salum anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Kamusoko Thaban
Dakika ya 70 Matheo Anthony almanusra aipatie Yanga bao kichwa chake kinaokolewa na Aron Kalambo
Dakika ya 73 Juma Abdul anatoka Anaingia Amis Tambwe
Dakika ya 74 Yanga wanapata penati
Goaaaaaal Ibrahim Ajibu anasawazisha bao kwa Njia ya penati
Mtu mzima Dawaaaaaaa ndivyo unaweza kusema Goaaaaaal Amis Tambwe anaipatia Yanga bao la pili
Dakika ya 85
Tanzania Prisons 1 – 2 Yanga
Dakika 3 zinaongezwa kumaliza Pambano
Goaaaaaal Tambwe tena, Tambwe Tena Anaipatia Yanga bao la Tatu baada ya Makosa ya James Mwasote
FULL TIME
Tanzania Prisons 1 – 3 Yanga (Ajibu, Tambwe 2)