Othman Kazi ataja watano waliostahili kadi nyekundu Prisons vs Yanga

Othman Kazi ataja watano waliostahili kadi nyekundu Prisons vs Yanga

0

 

Othman Kazi ataja  watano waliostahili kadi nyekundu Prisons vs Yanga

Mwamuzi mstaafu na moja kati ya waamuzi waliokuwa bora enzi zake Othman Kazi kupitia kipindi cha Kipyenga cha Mwisho kinachorushwa na Azam Tv amefunguka kuwa siyo wachezaji wawili pekee waliostahili kadi nyekundu katika mcezo kati ya Prisons na Yanga bali ni wachezaji watano.

Katika mcezo huo uliochezwa Jumatatu jijini Mbeya Ulishuhudia wachezaji Mrisho Ngassa na Lauren Mpalile wakipewa kadi nyekundu kutokana na vitendo visivyo vya kiungwana mchezoni.

Mrisho Ngassa alipewa kadi nyekundu kwa kumpiga Kichwa Hassan Kapalata wa Tanzania Prisons wakati Lauren Mpalile alikula umeme kwa kumshambulia Mrisho Ngassa kwa kumpiga Kichwa.

Kulingana na Othman Kazi amefunguka kuwa hata Kitendo cha Andrew Vincent kuonekana kumzonga Mwamuzi na Kumpiga kichwa kilistahili kadi nyekundu.

Ratiba mechi 2 za Leo ligi kuu Tanzania Bara TPL

Mwingine ni Heritier Makambo alionekana kufanya vitendo ambavyo vilistahili kadi nyekundu cha Kwanza ni kumpiga Kiwiko Lauren Mpalile wakati wa Vurugu za Ngassa na kitendo kingine Makambo alimkanyaga Mwamuzi makusudi wakati ambao wachezaji wa Yanga walikuwa wakilalamikia penati iliyotolewa na Mwamuzi Meshack Suda.

Mchezaji mwingine aliyestahili kupewa kadi nyekundu kulingana na Othman Kazi msomaji wa Kwataunit.co.ke ni Jumanne Elifadhili wa Tanzania Prisons ambaye alimkanyaga mchezaji Feisal Salum wakati ambao alikuwa tayari ameshapiga Mpira lakini Mwamuzi Meshack Suda aliishia kumpa kadi ya Njano katika mchezo huo.Ungana nasi KUPITIA App yetu ya Michezo >BONYEZA HAPA<

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY