Tambwe ammwagia sifa mchezaji huyu Yanga

Tambwe ammwagia sifa mchezaji huyu Yanga

0

Tambwe ammwagia sifa mchezaji huyu Yanga

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Amiss Tambwe, amesema licha ya kikosi chao kuwa na wachezaji makini, lakini Ibrahim Ajib ameweza kuwasaidia sana kufika walipo sasa.

Akizungumza na nasi, Tambwe alisema Ajib anastahili sifa kwani idadi kubwa ya mabao yaliyofungwa na timu yao chanzo ni yeye.

“Kuna kipindi nilikuwa nje ya uwanja lakini bado safu ya ushambuliaji ilionekana kufanya vizuri pasipo kuonyesha kuna mapungufu na hii ilitokana na Ajib kutengeneza muunganiko mzuri na Makambo.

“Siwezi kuacha kumpa sifa Ajib ambaye ameweza kuitendea haki nafasi anayocheza bila ya kujali anasaidiana na nani kubwa kwake ni Yanga kupata ushindi,” alisema Tambwe.

Mabingwa Klabu Bingwa Afrika toka 2003 mpaka 2018

Tambwe aliongeza: “Wachezaji wote wanajituma kulingana na nafasi zao lakini kwa Ajib mbali ya kufunga, ametoa pasi nyingi za mabao na bila shaka ndio anayeongoza katika upigaji wa pasi za mwisho katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.”

“Hata mabao anayoyafunga Heritier Makambo, asilimia kubwa Ajib ndiye ametoa pasi za mabao, kutokana na uwezo mkubwa alionao wa kupiga krosi na pasi nzuri ambazo anazitengeneza kwa wachezaji wote,” aliongeza Tambwe.

Katika mechi za Ligi Kuu, hadi sasa Ajib amefunga mabao matano sawa na Tambwe, huku akiwa ametoa pasi za mabao 12.

Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY