Tetesi za usajili Simba dirisha dogo leo 7 December 2018

Tetesi za usajili Simba dirisha dogo leo 7 December 2018

0

 

Tetesi za usajili Simba dirisha dogo leo 7 December 2018

Kiungo Mzambia Clatous Chama ‘CCC’ ni wa moto kwelikweli wakati huu kutokana na kiwango kikubwa anachoonyesha dimbani

Tayari timu nyingi kutoka Afrika na Ulaya zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo aliyetua Simba mwanzoni mwa msimu akitokea Dynamos ya Zambia

Wakala wake Faustino Mkandila amekiri Chama anawindwa na timu kadhaa kutoka Ulaya miongoni mwa timu hizo mbili kutoka nchi za Uturuki na Ubelgiji zikitaka kumsajili wakati wa dirisha dogo la usajili linalofunguliwa mwezi wa kwanza huko Ulaya.

Mkandila amesema amepokea ofa hizo na watakuwa tayari kumuuza Chama kwa timu itakayokubali kutoa kitita cha Dola Mil 2 (zaidi ya Bil 4.5 za Kitanzania)

Chama anakuwa mchezaji wa tatu kuingia katika rada za timu kadhaa zinazotaka kumzajili.

Mganda Emmanuel Okwi anawindwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakati Meddie Kagere anawindwa na vilabu vya Zamalek na AS Vital

Match Preview : Azam Fc vs Mbao Fc

Simba itaingiza kiasi kikubwa cha fedha kama itaruhusu kuuzwa kwa wachezaji hao.

Hata hivyo jambo hilo litakuwa la mwisho kabisa kutokea kutokana na umuhimu wao katika kikosi cha Simba ambacho msimu huu kimepania kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY