Tetesi za usajili Simba Dirisha dogo leo 8 December 2018

Tetesi za usajili Simba Dirisha dogo leo 8 December 2018

0

 

Tetesi za usajili Simba Dirisha dogo leo 8 December 2018

Ukizungumza timu ambazo zimekuwa na vikoso tishio kwasasa Afrika Mashariki ni wazi Simba ni moja ya timu zenye vikosi vya kutishia wapinzani wake.

Usifikiri ubora wa kikosi cha Simba unaonekana Tanzania pekee kwasasa , Ubora was kikosi cha Simba umekuwa ukichagizwa zaidi na Safu hatari ya Ushambuliaji inayoongozwa na Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco

Siku za Karibuni kumekuwa na Taarifa za wachezaji wa Simba kama Meddie Kagere na Emmanuel Okwi kutakiwa na Vilabu vya Afrika Kusini.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alipotafutwa kuzungumzia juu ya wachezaji hao na tetesi za Kutua Sauzi alifunguka kuwa kwasasa hawezi kukubali kuwaacha wachezaji hao watimke kwani anawaza kuwatumia vizuri kimataifa.

Aussems ameweka wazi kuwa wachezaji hao ni muhimu mno katika safu yake ya Ushambuliaji na anawategemea ili kuendelea kufanya vyema kimataifa hivyo hayuko tayari kuwaacha.

Licha ya kauli hiyo ya kocha mkuu msomaji wa Kwataunit.co.ke imekuwa ikielezwa kuwa kumekuwa na donge nono linalowekwa mezani na vilabu vya sauz kiasi cha kuwatamanisha wachezaji lakini pia mikataba ya wachezaji wengi wa Simba huwaruhusu wachezaji kuondoka wanapotakiwa na timu za nje ya nchi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY