Usajili: Kipa Prisons ataka Yanga ifanye kweli

Usajili: Kipa Prisons ataka Yanga ifanye kweli

0

 

Usajili: Kipa Prisons ataka Yanga ifanye kweli

KIPA wa timu ya Tanzania Prisons, Aaron Kalambo, amesema kama uongozi wa klabu ya Yanga unamhitaji kuziba pengo la mlinda mlango wao namba moja, Beno Kakolanya, wafanye kweli kwani yupo tayari kuitumikia.

Akizungumza na nasi jana, Kalambo alisema alipata ujumbe kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo kuwa wanamhitaji baada ya kucheza mechi dhidi yao wiki iliyopita katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

“Ni kweli nina taarifa kuwa Yanga wananitaka kama wanayo nia hiyo wanifuate mimi nipo tayari, ila jambo la msingi ni kufikia makubaliano,” alisema Kalambo.

Aidha, Kalambo alisisitiza kuwa lengo lake kubwa ni kupata timu ambayo itajali masilahi yake kwani bado yupo katika mbio za kutafuta maisha, pia aweze kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chake.

Hata hivyo, Kalambo alisema mpaka sasa bado uongozi wa Yanga haujamtumia ujumbe wowote kama kweli wana nia ya kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY