Wachezaji watakaokosekana na watakaorejea kikosini Yanga dhidi ya Biashara

Wachezaji watakaokosekana na watakaorejea kikosini Yanga dhidi ya Biashara

0

 

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mkongo, Mwinyi Zahera amesema anatambua mchezo unaoikabili timu yake Jumapili, Disemba 9 dhidi ya Biashara United ya mkoani Mara, ni mgumu kwakua anakutana na timu ilioko nafasi ya mwisho katika ligi.

Zahera amesema mara nyingi mechi za timu zilizo katika nafasi za mwishoni huwa ni ngumu kutokana na timu hizo kucheza kwa kujituma ili kujikwamua katika nafasi zilizopo.

“Najua mchezo wetu na biashara utakuwa mgumu sana , naelewa shida iliyopo pale tunapokutana na timu iliyo nafasi ya mwisho, huwa inajipanga kuhakikisha inapata alama tatu ili kujikwamua huko ilipo,” amesema Zahera.

Aidha Zahera amewataka wachezaji wake kupambana kufa kupona ili waendeleze rekodi nzuri waliyonayo ya kutopoteza mchezo wowote na kikubwa zaidi ni kuhakikisha wanajikusanyia alama tatu.

“Wachezaji wanapaswa kujitayarisha kisaikolojia nawaomba wawe na utayari wa kucheza mchezo huo, nitakuwa mkali sana kwa wachezaji wangu katika mechi hiyo, ” amesema Kocha huyo.

Zahera amesema Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu katika mchezo huo, Ibrahim Ajib(kadi Tatu za njano) na Mrisho ngasa (kadi nyekundu), aidha Papy Tshishimbi na Kelvin Yondani waliokosekana katika michezo mitatu iliyopita watakua ni sehemu ya kikosi kitakacho kutana na Biashara.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY