Zahera ashangazwa na Jambo hili Yanga

Zahera ashangazwa na Jambo hili Yanga

0

 

Zahera ashangazwa na Jambo hili Yanga

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewashangaa matajiri wenye mapenzi na klabu hiyo kwa kushindwa kuisaidia timu hiyo ambayo kwa sasa imekumbwa na ukata.

Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi 38 katika mechi 14 walizocheza, lakini taarifa ndani ya klabu hizo zinadai timu imekumbwa na ukata na kushindwa kulipa wachezaji mishahara ya miezi minne sasa.

Akizungumza nasi juzi kutokea mkoani Mbeya, Zahera alisema anashangaa timu hiyo kuishi kimasikini wakati ina wanachama ambao ni matajiri.

habari mpya Kutoka Yanga mchana wa Leo

Kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alikwenda mbali zaidi na kusema licha ya wanachama hao kushindwa kuisaidia timu hiyo, anashangaa wanaopiga hela kwa mgongo wa timu hiyo.

“Timu haina hela hilo lipo wazi, nawashangaa matajiri wenye mapenzi na hii timu wapo wapi, wao ndio wanaweza kuisaidia timu kutoka hapa ilipo.

“Si kwamba timu haiingizi hela, hapana, kuna wajanja wachache wanaendelea kuing’ang’ania timu mikoani, wanagombania ukuu wa msafara na kupiga hela ndefu ambazo zingeweza kutusaidia kulipana mishahara,” alisema.

Zahera alisisitiza kuwa kilichomleta Yanga si fedha bali ni kufundisha soka ikiwa ndiyo kazi yake, lakini pia kuendelea kuboresha wasifu (CV) wake, akiamini lazima ataipaisha Yanga.

“Nilipotua nakumbuka niliambiwa maneno mengi sana kuwa Yanga haina fedha hivyo ningetaabika sana, lakini hilo halinisumbui mimi kwa sababu nataka kuona Yanga inafanya vizuri,” alisema.

Source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY