Alichokisema Aussems baada ya 5 za As Vita

Alichokisema Aussems baada ya 5 za As Vita

0

Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kipigo cha mabao 5-0 walichopata kutoka kwa wenyeji AS Vita ni elimu kwao.

Aussems amesema Vita Club iliwazidi katika ubora na kuifanya timu yake kukubali kipigo hicho kikubwa zaidi kwako msimu huu.

Amesema wapinzani wao walikuwa bora zaidi kwa mchezaji mmoja mmoja hali ambayo iliwapa wakati mgumu kubadili matokeo.

Hata hivyo Aussems amesema licha ya changamoto hiyo bado suala la uamuzi wa mwamuzi hayakuwa sawa kutokana na kuwapendelea wenyeji.

Aidha Aussems amesema licha ya kipigo hicho kikubwa bado Simba inatakiwa kusahau haraka matokeo hayo na kuangalia mechi zilizombele yao ili waweze kufanikisha kuwa bora katika kundi lao.

Simba mchezo wake ujao itakuwa ugenini Misri kucheza dhidi ya vinara wa Kundi D na mabingwa mara nane wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly mechi itakayochezwa Februari 2.

Simba yaanza na viungo wanne

Katika mchezo wa jana usiku Simba ilianza na viungo wanne dhidi ya AS Vita Club.

Aussems alianza na viungo wanne lakini wawili James Kotei na Jonas Mkude wakiimairisha safu ya ulinzi wakati Mzamiru Yassin na Clatous Chama wakiwa na kazi ya kupandisha mashambulizi

Hata hivyo wakati Chama akiwa kama kiungo huru Mzamiru atakuwa na kazi ya kutokea pembeni kulia ingawa akiwa na kazi pia ya kushuka haraka kusaidia ukabaji wakati timu inashambuliwa.

Safu ya ulinzi ilikuwa na kipa Aishi Manula mabeki Nicholas Gyan kulia kushoto akiwa nahodha Mohammed Hussein kati wakiwa Juuko Murshid na Pascal Wawa, huku ushambuliaji ilikuwa chini ya Kagere na Okwi.

Source : Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY