Alichokisema Cannavaro kuhusu Yondani kutolewa unahodha

Alichokisema Cannavaro kuhusu Yondani kutolewa unahodha

0

Alichokisema Cannavaro kuhusu Yondani kutolewa unahodha

MENEJA wa timu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema kitendo cha kocha wao, Mwinyi Zahera, kumvua unahodha Kelvin Yondani ni sahihi kwa kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kukiongoza kikosi hicho.

Zahera alifanya uamuzi wa kumvua unahodha Yondani ambaye ni beki mkongwe ndani ya timu hiyo na kumkabidhi mikoba mshambuliaji, Ibrahim Ajib.

Inadaiwa uamuzi huo umefanyika baada ya mlinzi huyo kuonyesha utovu wa nidhamu.

Yondani alikabidhiwa kitambaa cha unahodha mwanzoni mwa msimu huu akichukua mikoba ya Cannavaro aliyestaafu soka na kupewa kazi ya umeneja.

Akizungumza na nasi kutoka visiwani Zanzibar, Cannavaro alisema mpaka kocha anafanya uamuzi wa kumvua unahodha mchezaji ni lazima atakuwa ameshakaa na kuzungumza naye, hivyo haitakiwi aonekane amefanya uonevu.

“Kocha ndiye mwenye mamlaka na timu hivyo kumvua unahodha Yondani isionekane kama amemwonea, nina uhakika pia ninatambua anachokifanya.

“Watu wengi wanahoji kwanini Ajib amepewa jukumu hilo, lakini ninaamini vizuri aachiwe kocha mwenyewe afanye kile anachoona kinafaa,” alisisitiza Cannavaro.

Like ukurasa wetu wa Facebook Hapa kwa habari zaidi

Install Simba na Yanga Breaking News App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY