Fei Toto afunguka kucheza pamoja na Boban

Fei Toto afunguka kucheza pamoja na Boban

0

Fei Toto afunguka kucheza pamoja na Boban

Kiungo wa klabu ya Yanga Feisal Salum maarufu pia kama Fei Toto amefunguka namna anavyojisikia akicheza na Kiungo Mkongwe Haruna Moshi Shaaban “Boban”

Feisal Salum amefunguka kuwa kucheza na Boban si jambo dogo kwake kwani mchezaji huyo ni mzoefu na amekuwa akijifunza mengi kila anapocheza naye uwanjani.

Moja kati ya vitu ambavyo Feisal Salum amevutiwa na Boban ni Utulivu mkubwa ambao amekuwa nao anapocheza.

“Kucheza pamoja na Boban si jambo dogo, ni mchezaji mwenye uzoefu anayenifunza vitu vingi haswa kwenye safu ya kiungo. Ana utulivu na mwenye kipaji cha aina yake akiwa analisakata gozi” alisema.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY