Habari 4 Kubwa za Michezo jioni ya Leo 29 January 2019

Habari 4 Kubwa za Michezo jioni ya Leo 29 January 2019

0

Habari 4 Kubwa za Michezo jioni ya Leo 29 January 2019

Arusha United yamtimua Kocha Minziro

Timu ya Arusha United “Wana Utalii” leo imetangaza rasmi kumtimua kocha wake Fred Felix “Minziro” kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri ligi daraja la Kwanza

Nafasi ya Minziro imechukuliwa na aliyekuwa kocha mkuu wa Singida United kabla ya Kubwagana nao Hemed Morocco.

NDIMBO AULA CAF

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo  kuwa Afisa Habari wa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas.

SIMBA YAPAA KUIFUATA AL AHLY

Klabu ya Simba jioni ya leo imepaa kuifuata Al Ahly ya Misri huku kikosi cha Simba kikiwa na Nahodha wao aliyekuwa nje kwa mechi kadhaa John Raphael Bocco ambaye amejumuishwa.

Kocha Wa Simba Patrick Aussems msomaji wa Kwataunit.co.ke amefunguka haya kabla ya kuondoka kwenda Misri.

“Tunakwenda kucheza na timu bora ila tutaingia kwa tahadhari kubwa na lengo letu litakuwa ni kushambulia na kujilinda kwani tukisema tujilinde muda wote itakuwa hatari kwenye lango letu.

“Uwepo wa Bocco ndani ya kikosi chetu unaongeza nguvu kwani wachezaji wangu wote siku zote huwa nasema wana uwezo mkubwa ila wanasumbuliwa na tatizo la kukosa umakini wakiwa eneo la hatari imani yangu tatizo litatapata tiba,”

Install App bora ya Michezo Tanzania

BENO KAKOLANYA AANZA MAZOEZI

Kipa wa timu ya Yanga ambaye amekuwa nje ya Kikosi kutokana na kocha wa Yanga Zahera mwinyi kutomtaka katika kikosi chake Beno Kakolanya ameanza mazoezi katika Gym moja jijini Dar Es Salaam mitaa ya Manzese.

Inaelezwa kuwa Beno anafanya mazoezi ili kutoua kipaji chake kutokana na kukosa nafasi ya Kucheza kwa Muda.

Install App bora ya Michezo Tanzania

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY